
Benki ya NMB imetangaza udhamini wa Sh milioni 150 kwa msimu wa nane wa Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi—CDF Cup 2026, yatakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Julai 6 hadi 17. Mashindano haya yatashirikisha michezo 13 na timu kutoka sehemu mbalimbali za JWTZ. Aikansia Muro, Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa NMB, alisema udhamini huu unaimarisha ushirikiano kati ya benki na majeshi katika kukuza michezo.