
Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na uongozi wa chama tawala cha Labour, akisema atasalia madarakani hadi kiongozi mpya atakapopatikana. Starmer amekumbana na kashfa na migogoro ya kisera, huku wabunge wa chama chake wakimlaumu kwa maamuzi yasiyokubalika na wananchi. Waziri Mkuu ajaye atakuwa kiongozi wa saba wa Uingereza ndani ya kipindi cha miaka 10.