
Taasisi zinazohusiana na sekta ya ubaharia nchini Tanzania zimehimiza kuimarisha ushirikiano ili kusaidia wahitimu kupata ajira kwenye meli na kuchangia ukuaji wa sekta hiyo. Wito huu ulitolewa na Father Johnson Lameck wa Taasisi ya Mission for Seafarers wakati wa maadhimisho ya Siku Maalumu ya Kuwakumbuka na Kuwaombea Dua Mabaharia, ambapo alisisitiza umuhimu wa bahari na fursa za uchumi wa buluu nchini.