
Rais wa Namibia, Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania tarehe 19 Juni 2026 kwa ziara ya kitaifa, ambayo ni ya pili tangu aingie madarakani mwaka 2024. Katika ziara hiyo, atafanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu ushirikiano wa pande mbili na masuala ya kikanda na kimataifa. Aidha, atatembelea eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam, ambapo aliishi miaka ya 1980.