
Profesa Henry Mollel, Rais wa Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Mbeya, amesema kuwa David Kafulila, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-Centre), ameleta mabadiliko makubwa ya fikra nchini kuhusu utekelezaji wa PPP, hatua inayochochea matumizi ya ubia huo.

