
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesema Serikali inatumia mikopo nafuu ili kuharakisha maendeleo ya miundombinu ya kisasa nchini, ikiwemo barabara na viwanja vya ndege. Katika mchango wake kuhusu Bajeti ya Serikali ya mwaka 2026/2027 bungeni, Ulega alisisitiza kuwa mikopo hiyo imeleta matokeo makubwa yanayoonekana kwa wananchi, akipinga kauli za baadhi ya viongozi kuhusu suala hilo.