
Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kimejipanga kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuzalisha watumishi wenye weledi kupitia ufundishaji, tafiti, na kuandaa wataalamu. Mkuu wa chuo, Profesa Hozen Mayaya, alieleza kuwa chuo kinaendelea kuandaa rasilimali watu wenye ujuzi na uwezo wa kufanya kazi katika taasisi za serikali na sekta binafsi, akisisitiza umuhimu wa rasilimali watu katika kufanikisha Dira hiyo.