
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ametoa miezi mitatu kwa mkandarasi anayejenga barabara ya Mnivata – Mitesa yenye urefu wa kilometa 100, kuhakikisha wanakamilisha kilometa 50 za barabara hiyo kwa kiwango cha lami. Agizo hili lilitolewa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara, lengo likiwa ni kuufungua Mkoa wa Mtwara kiuchumi na kuunganisha Wilaya mbalimbali za mkoa huo.
