Michuzi Blog·12d ago
.jpeg)
Wananchi na wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wamepongeza Mfumo wa Kujihudumia Binafsi unaowezesha kupata huduma kupitia simu janja, wakisema mfumo huo umeongeza uwazi, ufanisi, na kuokoa muda wa kupata huduma. Wamesema hayo walipotembelea banda la NHIF katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.